Karibu mahali penye utulivu, kwa sala na tafakari.
Hii ni Nyumba ya Sala iliyopo kandokando ya Ziwa Victoria. Hapa tunakaribisha mtu binafsi au kikundi kinachotafuta muda wa kujitenga na shughuli za kila siku ili kupumzika, kusali, kutafakari na kuanza upya.
Kuna nyakati ambapo tatizo si kukosa majibu, bali kukosa utulivu wa kuyasikia.
Maisha yanapoenda kwa kasi, huwa rahisi kupoteza nafasi ya kupata utulivu wa kukuwezesha kusali, kuomba na kutafakari mapito katika maisha yetu ya kila siku. Si kwa sababu majibu hayapo, bali kwa sababu ya mahangaiko mengi na kelele za kila siku kwenye maisha yetu, huzidi ukimya tunaouhitaji kutafakari na kupata majibu haya.
Kwa sababu hiyo, Nyumba ya sala Ziwani ipo kutoa nafasi hii kukuwezesha wewe kupata utulivu unaohitaji na kuwa karibu na Mungu. Wengi hufika wakiwa wamechoka na hutafuta fursa ya kuweza kufanya uamuzi muhimu maishani mwao.
Vilevile wapo wanaohitaji muda wa sala baada ya kipindi kigumu maishani. Na wengine huja kwa sababu wanahitaji kutulia tu kwa muda mfupi na waweze kurejea kwenye shughuli za kila siku.
Huduma Zetu
Watu huja kutafuta muda wa kuwa peke yao mbele za Mungu. Wengine wanahitaji utulivu wa sala na tafakari baada ya shughuli nyingi za maisha au kazi. Wapo wanaofika wao binafsi, na wengine huja kama jumuiya, vyama vya kitume au vikundi vikubwa na vidogo kwa sala na mafungo ya siku moja ama zaidi.
Wengine hutafuta mwongozo wa kiroho. Wengine hutafuta ukimya. Wengine huja ili wapumzike tu na kurejea kwenye utaratibu wa maisha wakiwa na ufasaha zaidi.

Mafungo ya mtu binafsi
Unaweza kuja kwa siku moja au kukaa kwa siku kadhaa. Ratiba ni rahisi, ikiwa na muda wa sala, Misa, chakula na ukimya. Muda uliobaki ni wako, kwa ajili ya kusoma, kutafakari, kusali ama kupumzika.
Ukihitaji, unaweza kupata mwongozo wa kiroho kutoka kwa mmoja wa waongozaji wetu.
View Details→

Mafungo ya kikundi
Tunapokea parokia, jumuiya, mashirika, shule na vikundi vinavyotafuta mazingira ya utulivu kwa ajili ya mafungo au siku za sala na tafakari.
Mnaweza kuja kwa siku moja au kukaa kwa siku kadhaa, na kupanga ratiba yenu kulingana na malengo ya kikundi chenu.
View Details→
Gharama
Kwa Kulala
Sh 60,000
Kwa mtu mmoja kwa usiku. Bei inajumuisha kifungua kinywa, chakula cha mchana na cha jioni.
Kwa Kutwa
Sh 10,000
Kwa mtu mmoja. Bei inajumuisha chakula cha mchana. Kwa vikundi vikubwa, tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.
Wote wanakaribishwa
Nyumba ya Sala Ziwani ni kituo cha mafungo na sala cha Kanisa Katoliki kinachofuata utamaduni wa sala na tafakari wa Mtakatifu Inyasi wa Loyola.
Tunathamini ukimya, sala, tafakari na usikivu wa ndani. Ingawa msingi wetu ni wa Kikatoliki, tunawakaribisha watu wa imani mbalimbali wanaoheshimu mazingira ya utulivu na sala.
Tunapatikana Kahuboro-Ibanda, Wilaya ya Ilemela, Mwanza, mkabala na shule ya sekondari ya Kirumba juu ya kilima kinachoangalia Ziwa Victoria.
Karibu wakati wowote
Wakati mwingine unahitaji siku moja tu ya utulivu. Wakati mwingine unahitaji zaidi. Ukiwa tayari, tutafurahi kukukaribisha Nyumba ya Sala Ziwani
